We have updated our Privacy and Cookie Notice to keep you informed where we may process your personal data. See more here or contact us for more information.

VIGEZO NA MASHARTI YA MPANGO WA NYANYUA BAA NA SERENGETI PREMIUM LAGER

1. Serengeti Breweries Limited (Ikijulikana pia kama “Sisi” au “SBL”), inaahidi kusaidia baa zinazoendelea na biashara kufainikisha biashara zao katika miji ya Dar es Salaam pamoja na Znzibar, Mwanza na Arusha kwa kipindi cha miaka miwili ijayo

2. Tutatumia kiasi cha fedha kilichoahidiwa kusaidia mambo mbali mbali kwa biashara zinazoendelea na ambazo tutazichagua. Msaada utatolewa kwa hatua ukianzia na siku ya kanza (kama itakavyoshauriwa na sisi) na tutatangaza aina tofauti tofauti za misaada tutakayotoa kupitia tovuti ya www.diageobaracademy.com (DBA). Tutakuwa tukifanya tathmini ya mara kwa mara kuona namna bora zaidi ya kusaidia biashara zinazoendelea na tunaweza kubadilisha aina za misaada tunayotoa.

3. Ili kuweza kupokea msaada (Mwombaji au wewe) ni lazima:

4. Ni lazima ufuate maelekezo unayopewa na sisi (kupitia tovuti ya DBA, barua pepe au njia nyinginezo) ili kuomba msaada na tunaweza kuhitaji ushahidi wa kuonyesha kuwa unastahili kupata msaada husika.

5. Kutakuwa na kiwango kwa kila aina ya msaada utakaotolewa. Pia, kutakuwa na ukomo wa kiasi ambacho kila mhitaji anaweza kuomba ambacho kitaelezwa kwenye DBA au kwenye maelezo utakayopata wakati misaada itakapotangazwa. Hautakiwi kwa namna yotote ile kujaribu kuzidisha kiwango kilichowekwa.

6. Tutatoa msaada lakini msaada huu utatolewa na watu au kampuni nyingine kwa niaba yetu (Wazabuni)kwa waombaji wataokidhi vigezo. Kila atakayekuwa anatoa msaada kwa niaba yetu atawajibika kwa msaada atakaokuwa anautoa na sisi hatutawajibika kutokana na upotevu au uharibifu utakaotokana na msaada unaotolewa kwa niaba yetu.

7. Ni lazima ufuate maelekezo yote, muongozo na vigezo yanayoendana na vifaa au huduma zitakayotolewa na kampuni/watu watakaoekuwa wakitoa msaada kwa niaba yetu. Utawajibika kuvitunza na kuvitumia vizuri vifaa vyote au huduma utakazopewa kama sehemu ya msaada.

8. Ni lazima ufuate kikamilifu sheria husika, taratibu na mwongozo wa mamlaka zozote za udhibiti zitakazokuwa zinahusika katika matumizi ya msaada huu.

9. Hautakiwi kuuza au kujaribu kuuza vifaa vyovyote au huduma uliyopokea ikiwa kama sehemu ya masaada.

10. Utawajibika kulipa kodi aina zote pamoja na gharama nyinginezo zitakazotokana na kupokea na kusambaza msaada husika. Kutakuwa hakuna fedha sawa na masaada husika zitakazokuwepo. Msaada hauwezi kubadilishwa kwa aina nyingine ya msaada au thamani yake kwa fedha taslimu na pia hauwezi kuuzwa.

11. Kama utafanikiwa kupata msaada na ukashindwa kuchukua msaada huo ndani ya muda uliowekwa, tutafanya jitihada za kukufikia na kukusaidia kufanya utaratibu wa kuchukua msaada husika na endapo tutashindwa kukufikia au kukupata, tunaweza kukuondoa kwenye utaratibu wa kushiriki kwenye Mpango wa Ahadi za Kuyasaidia Mabaa kunyanyuka.

12. SBL inaweza kuondoa au kubadilisha vigezo vya Mpango wa Ahadi za Kusaidia Mabaa Kunyanyuka wakati wowote ndani ya kipindi cha mpango huu endapo kutatokea jambo lolote ambalo halikutarajiwa na ambalo ni nje ya uwezo wake bila kuhusisha gharama au uwajibikaji kwa upande wetu.

13. SBL inaweza kuvunja au kusitisha kwa muda mkataba wa Kusaidia Mabaa Kunyanyuka endapo litatokea tukio lolote linaloweza kufanya utekelezaji wake kuwa mgumu au kinyume na matarajio.

14. SBL inaweza kurekebisha vigezo hivi na masharti mara kwa mara kwa kutuma mabadiliko kwenye tovuti ya Diageo Bar Academy.

15. Endapo kutakuwa na sababu yoyote ya kufanya tuamini kuwa kuna uvunjifu wa vigezo na masharti, SBL inaweza kuwaondoa waombaji kushiriki kwenye Mpango wa Kuyanyanyua Mabaa bila gharama zozote au uwajibikaji kwa upande wetu.

16. SBL inaweza kutumia taarifa binafsi utakazotoa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Nyanyua Baa na Serengeti Premium Lager na pia tunaweza kumpatia mtu au kampuni inayotoa misaada hiyo kwa niaba yetu. Taarifa binafsi zitatumika kwa mujibu wa sera ya usiri ya Diageo ambayo unaweza kuipata kupitia tovuti ya Sera ya usiri ya.

17. Kwa kukubali kushiriki kwenye Mpango wa Nyanyua Baa na Serengeti Premium Lager, umekubali kupokea taarifa zaidi kwa njia ya barua pepe/posta juu ya mpango huu au mafunzo ya Diageo Bar Academy. Unaweza kuamua kujiondoa katika utaratibu wa kupokea taarifa hizi muda wowote utakapoamua kwa siku zijazo.

18. Hutakiwi kutumia chapa au haki miliki za SBL au washirika wake au kufanya matangazo yoyote au machapisho kuhusiana na www.DrinkiQ.com